×

Wanawake Matajiri Zaidi Afrika, Cha Kujifunza Kutoka Kwao

Wanawake matajiri wanazidi kujitokeza barani Afrika.  Je, nini tunaweza kujifunza kutoka kwao?
Folurunso Alakija – Nigeria 🇳🇬

Richest women in Africa

Ni mmoja wa wanawake matajiri zaidi wa Afrika, akiwa Mtendaji Mkuu wa kampuni la mafuta la Famfa la Nigeria na ana utajiri wa Dola bil. 1.6 (Sh. tril. 3.6) .  Pia ana biashara kubwa za mambo ya fasheni na viwanda vya uchapaji.  Alipata utajiri kwa kuwekeza katika biashara ya mafuta kupitia ushauri wa rafiki yake.

Hivyo, ni vyema kuzitumia fursa zozote za kuwekeza, na rafiki wa kweli ni yule anayekupa ushauri wa kufanikiwa maishani.

Hajiya Bola Shagaya – Nigeria 🇳🇬

Richest women in Africa

Hajiya Bola Shagaya, wa Nigeria, ni mmoja wa wanawake matajiri wakubwa  wa Afrika kwa kuwekeza katika miradi mingi ya majengo barani Ulaya na Marekani, katika miradi ya mafuta, benki, mawasiliano, na kadhalika.  Ana utajiri wa Dola mil. 630 (Sh. bil. 1.4).

Cha kujifunza ni kuwekeza sehemu mbalimbali na “si kuyaweka mayai yote katika kikapu kimoja”, kwani yanaweza kuvunjika yote.

Ngina Kenyatta – Kenya 🇰🇪

Richest women in Africa

Mama Ngina ana umri wa miaka 85, ni mjane wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.  Ana hisa kubwa katika moja ya mabenki makubwa zaidi nchini Kenya, kwenye mahoteli, majengo na ardhi, viwanda vya maziwa, vyombo vya habari, mbao na kadhalika, vyote hivyo kumfanya awe na utajiri wa Dola bil. 1 (Sh. tril. 2.3).

Kuwekeza katika miradi mingi kunalipa.

Bridget Radebe – South Africa 🇿🇦

Richest women in Africa

Bridget Radebe ni raia wa Afrika Kusini aliyezaliwa 1960, ni mwasisi wa kampuni kubwa la madini nchini humo liitwalo Mmakau Mining, ambalo linajihusisha na uchimbaji wa dhahabu, platinum, uranium, makaa, na kadhalika.

Ana utajiri mkubwa unaofikia Rand bil. 2.

Mafanikio hayajali jinsia — mwanamke au mwanamme.