×

MASHABIKI WA SIMBA,YANGA WACHANGAMKIA GAZETI LA SPOTI XTRA

Mmoja wa wasomaji wa Gazeti la Spoti Xtra (kushoto) akijaza kuponi ya shindano la kujishindia jezi orijino au zawadi nyingine nyingi.

Mmoja wa maofisa usambazaji wa Gazeti la Spoti Xtra la Global Publishers (kulia) akimwonesha msomaji namna ya kushiriki  shindano hilo kwenye kuponi iliyopo kwenye gazeti hilo.
Wasomaji wakihamasika kutazama sehemu ya kujaza kuponi kwa ajili ya shindano hilo.
Msomaji wa  Spoti Xtra akijaza kuponi.
Mashabiki wa Klabu ya Simba wakishikilia Spoti Xtra baada ya kulinunua eneo la Uwanja wa Taifa kabla ya mechi kuanza leo jioni.

 

MAPEMA leo katika jiji la Dar es Salaam, eneo la Uwanja wa Taifa,  mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wamelichangamkia gazeti la Spoti Xtra linalotoka kila Jumaili kwa bei ya Sh.500/= na kujaza kuponi za shindano la kujipatia zawadi za jezi orijino na zawadi nyingine mbalimbali.

 

Kikosi kazi cha promosheni ya Spoti Xtra leo kiliendelea kulinadi gazeti hilo kwa wasomaji ambapo lilipita sehemu mbalimbali na kisha kutua Uwanja wa Taifa ambapo kuna  mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yanga.

 

Picha: Richard Bukos.