
RAIS John Magufuli ametoa shilingi milioni 20 na mkewe Janeth Magufuli ametoa shilingi milioni tano kwa wajasiriamli wa Feri Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam aliokutana nao jana wakati akifanya mazoezi.
Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) Amir Amani na kiongozi wa kina mama, Ashura Seif Nanjonga.
