
Abba Marcus Mayanja, mtoto wa mwanamuziki maarufu wa Uganda, Joseph Chameleone Mayanja, ameumia kidole cha mguu wakati akicheza soka nchini Marekani ambako baba yake yuko katika ziara ya muziki.
Chameleone yuko Marekani na watoto wake wawili wa kiume, Abba na Alpha.
Baada ya kufanyiwa upasuaji wa kidole hicho, baba yake na mama yake aitwaye Daniella Atimango Mayanja, walimpongeza kwa kuhimili tiba hiyo na kumtaka awe makini na miguu yake.

Marcus ni mwogeleaji mahiri ambaye ameiwailisha nchi yake mara nyingi na kushinda medali kadhaa, mbali na kujaribu kujikita katika muziki kama baba yake, darasani analimudu vyema somo la hisabati.
