MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameamua kufanya kitu cha kipekee katika wiki ambayo anakumbuka siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’.
Staa huyo ambaye jana Oktoba 2, 2018 ndiyo ilikuwa Birthday yake amepanga keshokutwa Ijumaa atatoa misaada kwa watoto, akina mama na vijana wa Tandale jijini Dar es salaam ambako ndiko alikozaliwa na kukulia.
“Jambo la kwanza kabisa ni kuzungumza na vijana wenzangu wa Tandale na kuwapa maneno fulani ya kuwatia moyo. Siku hiyo nitatoa bima ya afya kwa watoto sio chini ya 300, tunatoa mitaji kwa akina mama wasiopungua 200 wa pale Tandale. Kwa hiyo birthday yangu nitakuwa naisherekea hivyo,” amesema Diamond.
Aidha, msanii huyo amesema kuwa atatoa bodaboda 20 kwa vijana ambao hawana ajira pamoja na kukarabati baadhi ya shule za maeneo ya nyumbani kwao Tandale.