
MREMBO aliyewahi kushikilia Taji la Miss Mara mwaka 2000, Rashida Wanjara hivi karibuni alizua gumzo la aina yake baada ya picha akibusiana kimahaba na mwanamke mwenzake kuzagaa mitandaoni na kuzua utata.
Picha hiyo inayomuonesha Wanjara akibusiana na mwenzake ilizua maswali kwa baadhi ya watu wakidai inawezekana wawili hao wanacheza mchezo mchafu wa usagaji. Za Motomoto News ilimtafuta Wanjara ambaye alifunguka kuwa picha hiyo kwake ni ya kawaida kwa sababu ni rafiki yake wa kawaida na hao wanaowaza vibaya ni fikra zao hawezi kuwazuia.

“Huwezi kuwazuia watu kufikiria vile wanavyotaka, kumbusu mwanamke mwenzangu ni jambo la kawaida sana na hakuna kitu kingine cha zaidi na hakuna ajabu yoyote,” alisema Wanjara.