×

BET Wafunguka Upigaji Kura Wasanii Wanaowania Tuzo

Baada ya kuwepo kwa mkanganyiko juu ya upigaji kura, Kampuni ya BET imejitokeza na kufunguka kuwa kuwa hakuna tukio la upigaji kura kwa wasanii wanaowania tuzo hizo.

 

Tangazo hilo limechapishwakwenye mitandao ya kijamii kupitia BET Africa.

Hii imekuwa kinyume na matarajio ya watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambao waliamini kuwa upigaji kura utafunguliwa.

“There is no voting available except for the best new international category which closed on 11th of June,” ilisema taarifa kutoka BET Africa.

 

Tuzo za BET hapo awali ziliagiza watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia sehemu ya maoni ya machapisho yao kupiga kura kwa wagombea wao wanaowapenda.

 

Katika Kipengelea cha Best International Act, wanamuziki watatu kutoka Afrika wameorodheshwa ambao ni Diamond Platnumz, Burna Boy na Wizkid.

 

Nchini Tanzania, Diamond Platnumz amepokea lawama na ukosoaji kwa kuteuliwa kwenye Tuzo za BET.

Sehemu ya Watanzania ilizindua ombi kwenye mitandao ya kijamii kutaka Diamond Platnumz aondolewe kwenye Tuzo za BET. Ombi hilo hata hivyo, halikufanikiwa.

 

Diamond amejitokeza na kusema kuwa anaheshimu maoni ya kila mtu pamoja na wale wasiomuunga mkono.

STORI; SIFAEL PAUL | GPL

Leave a Comment