MWIGIZAJI maarufu Diaries Aliiptisam, a.k.a Sicho amethibitisha hulala na wanaume na wanawake. The Real Arab Princess kama anavyojiita, ambaye ni Raia wa Kenya anayeishi jijini Nairobi aliweka wazi mtindo wake alipokuwa akizungumza na mashabiki mtandaoni na kuanika hayo alipoulizwa swali na shabiki katika mtandao wa Instagram.

“Are you Bisexual?” aliulizwa ambapo ajibu hata bila kufikiria kwa kusema ”Sometimes,” kumaanisha hata wanawake anaweza kufanya mapenzi nao.

Alisema hivyo wiki chache baada ya kushukiwa kuwa hufanya vitendo vya usagaji baada ya kuonekana akiwapiga busu wanawake na wanaume.