×

RATIBA YA KUAGA NA KUZIKA MWILI WA MTOTO WA MWAKASEGE

Ratiba ya Kumuaga mtoto wa Mwalimu Christopher Mwakasege, Joshua Mwakasege aliyefariki Alhamisi October 11 :-

 

Mwalimu atawasili Dar leo Jumatatu, Jumanne mwili utaagwa Mbezi Beach Lutheran Church, Jumatano alfajiri ni safari kuelekea Mbeya, na Alhamisi ni mazishi Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.

Mahali ulipo msiba; Msiba uko Dar kwa mdogo wake Mwalimu Mwakasege anaitwa Eng. Mwakasingila (Mzee wa kanisa wa KKKT Mbezi Beach).

 

Jinsi ya kufika msibani; Fika hadi Mbezi Beach Jogoo, unaingia barabara ya Karibu Art Gallery kuelekea TAG Mbezi beach kisha utaona vibao vinavyoelekeza msiba ulipo.

 

Ratiba ya Jumatatu; Kutakuwa na sala ya pamoja na Mwalimu Mwakasege na familia yeke yote itakayofanyikia hapa msibani itakayoanza saa moja jioni, 7pm itakayoongozwa na Askofu , Mchungaji kiongozi na watumishi wengine.

 

Kuaga; Mwili wa marehemu utaagwa Jumanne 16 Oct kanisani KKKT Mbezi Beach Dar, kuanzia saa nane mchana (2pm), kaada ya kuaga mwili utapelekwa airport kwa ajili ya maandalizi ya safari.

 

Kusafirisha: Mwili utasafirishwa Jumatano 17 Oct kwa ndege

Mazishi: Yatafanyika alhamisi, Tukuyu, Mbeya 18 Oktoba,2018.

Muhtasari: Joshua alifariki ghafla baada ya kudondoka Alhamisi, Oktoba 11, 2018 akiwa kazini kwake World Bank Dar. Alikimbizwa Aga Khan hospital ila alifariki siku hiyo hiyo.