IKIWA ni takribani siku 9 tangu kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji (MO) na hatimaye kupatikana usiku wa kuamkia leo baada ya kutelekezwa na watekaji hao katika maeneo ya Viwanja vya Gymkana jijini Dar es Saalam, mfanyabiashara huyo amelieleza jeshi la Polisi namna ambavyo alitekwa.
Hapa ni eneo la tukio ambapo Mo alitelekezwa na watekaji hao maeneo ya Gymkana jijini Dar es Salaam, jeshi la polisi limefika eneo la tukio, uopekuzi na uchunguzi unaendelea kwenye gari lililotumika kumteka Mo.