Rais Samia: Katiba Mpya ni Suala la Muda Kutatangaza Kamati
Global Publishers March 8, 2023 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) pamoja na Wanachama wa Chama hicho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Maridhiano kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe aliyeikabidhi kwa niaba ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, pamoja na viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.Viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Moshi mkoani Kilimanjaro katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2023.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema muda sio mrefu ataunda kamati kwa kushirikiana na vyama vingine vya siasa ambayo itashughulika na suala la katiba mpya.
Akizungumza leo Machi 8, 2023 kwenye Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani wa Chadema, Rais Samia amesema suala hilo hakuna anayelipinga.
“Swala katiba hakuna anayekataa hata chama changu hakuna anayekataa, na muda si mrefu tutatangaza kamati ambayo itashughulikia jambo hilo”.amesema Rais Samia.
Kiongozi huyo wa nchi amesema kuwa “Hakuna kisichowezekana kwa mazungumzo, tulishuhudia nchi kadhaa ziliingia kwenye vita hakukupatikana suluhu, lakini suluhu ikaja kupatikana kwa mazungumzo”.