
Kampuni inayojishughulisha na masuala ya Masoko, Matangazo na Uandaaji wa Matukio ya JSP Marketing Link Limited ya Jijini Dar es salaam imeibuka Mshindi wa Tatu katika tuzo za kila mwaka za makampuni bora 100 hapa nchini.
Tuzo hizo zimetolewa Alhamis ya tarehe 25 Oktoba 2018 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe. Tuzo hizo zinasimamiwa na Kampuni ya KPMG wakishirikiana na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd huku lengo likiwa ni kutambua mchango wa kampuni za Saizi ya Kati zinazotoa huduma mbalimbali hapa nchini.
Katika Tuzo za mwaka huu Kampuni ya JSP Marketing Link Limited imeibuka mshindi wa nafasi ya tatu kati ya kampuni 100 katika tuzo hizo kutokana na ubora wa huduma zake kwa Watanzania, kampuni za kitaifa na kimataifa.

Tuzo za makampuni bora 100 ya Saizi ya kati hutolewa kwa lengo la kuongeza chachu ya utoaji huduma bora kwa wananchi, lakini pia hutumika kama kipimo cha kutambua mchango wa kila kampuni kwa Watanzania.
JSP Marketing Link Limited ni kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010 na imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma Bora katika sekta ya Masoko, Matangazo na Uandaaji wa Matukio mbalimbali yenye mlengo wa Kijamii na Kibiashara.

Kama kampuni tunapenda kuwashukuru waandaaji na wadhamini wa tuzo hizi, wateja wetu, wafanyakazi na waliokuwa wafanyakazi wa JSP Marketing Link Ltd tangu ilipoanzishwa pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.