×

Avuna Mil. 300 Kwa Mwaka Kwa Kuuza Soksi Zake Chafu

ROXY SYKES (33) mkazi wa Jiji la London, Uingereza, amefichua kwamba anajipatia kiasi cha Paundi 100,000 (Sh. milioni 300 kwa mwaka) kwa kuuza soksi zake zinazonuka kwa watu wanaopenda na kuabudu miguu.

Mwanamke huyo alianza biashara hiyo baada ya mtu mmoja kumdokeza kwamba alikuwa na miguu ya kuvutia ambapo aliamua kuanzisha ukurasa  katika mtandao wa Instagram ili kuthibitisha hilo kwa kuweka picha za miguu yake ambapo alipata wafuasi zaidi ya 10,000 katika mwezi mmoja waliomwambia ukweli wa jambo hilo.

Pamoja na watu kuipenda miguu yake na kumlipa kupitia picha alizowatumia, walimwomba pia awatumie vitu vinavyohusiana na miguu yake; hivyo alianza kuwatumia viatu vyake alivyokuwa anavaa na soksi.

Soksi hizo chafu zilinunuliwa kwa Paundi 20 (Sh. 60,000), viatu Paundi 200 (Sh. 600,000), hivyo kumwingizia Paundi 8,000 (Sh. mil. 24) kwa mwezi.

Roxy hakutaka kuwatumia picha yake kwani alijua walichokuwa wanakitaka ni miguu yake tu.

Hivyo, pamoja na kufanya kazi, bado anatumia muda wake mwingi kupiga picha za miguu yake na kuwatumia watu ambao huzinunua, ikiwa ni pamoja na viatu na soksi zilizochafuka na kunuka, anazozivaa.  Vyote hivyo vinamwingizia fedha ya uhakika na ya kirahisi kila mwezi!