MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Jumapili ya Novemba 04, amejikuta akimwaga machozi mbele ya madhabahu ya Kanisa la Efata Ministry lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam wakati akifanyiwa toba na Mchungaji wa Kanisa hilo, Josephat Mwingira.
Akizungumza kanisani hapo, Rc Makonda, amesema anamshukuru sana Mungu kwa kuendelea kumlinda mpaka leo yupo hai kwani changamoto za kazi yake ni kubwa sana na maadui ni wengi, huku akisema amefika kanisani hapo kwa ajili ya kufanya toba kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Baada ya kuzungumza Rc Makonda, akafanyiwa maombi ya ulinzi wa Mungu kutoka kwa Mchungaji Josephat Mwingira.