MWANAMUZIKI nyota wa Nigeria, Wizkid, ameripotiwa kununua gari mpya aina ya Lamborghini Urus kwa Naira milioni 101 ambazo ni sawa na Sh. milioni 633. Habari hizo zinakwenda sambamba na video inayotesa hivi sasa ikimwonyesha katika gereji moja akilikagua gari hilo.
Wizkid hivi karibuni ametoa video yake iitwayo `Fever’, ambayo ilitusua vilivyo kwenye mtandao wa Intaneti na kutazamwa na watu zaidi ya milioni mbili katika saa zisizozidi 48.
Katika mazingira hayo, amejiunga na orodha ya wasanii wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi duniani hususan pale alipotoa shoo katika moja ya makazi maarufu zaidi duniani — Umaid Bhawan Palace nchini India.
Katika shoo hiyo alilipwa Rupee milioni 50 ambazo ni sawa na Naira ilioni 245.9, kiasi ambacho hapa nyumbani ni sawa na Sh. bilioni 1.5. Katika shoo hiyo kwenye harusi, aliwafanya Wahindi wacheze midundo ya nyimbo zake maarufu kama vile “Soco’’, “Fake Love’’ na nyingine nyingi.