Naibu Spika Dk Tulia Ackson, amemtoa nje Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa wakati wabunge wakichangia Azimio la kumpongeza Rais kuhusu uamuzi wa serikali kununua korosho za wakulima.
Uamuzi wa Naibu Spika umefuatia mabishano baina yake na Mchungaji Msigwa baada ya kumtaja Mbunge huyo kuwa alikuwa anapiga kelele.
Dk Tulia alimuonya zaidi ya mara tano kumtaka Msigwa akae chini lakini Mbunge huyo aligoma ndipo akamtaka atoke nje na alipogoma aliwaita askari wamtoe nje na wakatekeleza.