×

Waziri Mkuu, RC Makonda Walivyofika MSIBA WA RUGE MUTAHABA – Video

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa Serikali ambao wamefika katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba aliyefariki dunia jana nchini Afrika ya Kusini.

 

Majaliwa amefika msibani hapo ambapo ni kwa baba yake na Ruge, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

“Marehemu ndani ya Serikali amefanya kazi kubwa sana kwa kutafsiri philisophia ya viongozi wetu. Alianza awamu ya Nne (chini Rais Mstaafu Dkt Kikwete) na awamu hii ya tano… Amefanya kazi kubwa ya kuelimisha, ametoa mchango mkubwa wakati mwingine hata wa fedha zake…” 

 

“Jambo hili ni kubwa kwetu Watanzania, jambo hili ni kubwa kwetu ndani ya Serikali. Hivyo natoa pole kwa Watanzania wote. Nasema hivyo kwa sababu Watanzania wote tunafahamu mchango wake,” amesema Majaliwa wakati akumzungumzia marehemu Ruge.

Viongozi wengine waliofika ni Makamu wa Rais Mstaafu, Dk Mohamed Gharib Bilal, Naibu Spika, Dk Tulia Ackosn, Mbunge Mwigulu Nchemba, Zitto Kabwe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani ManyaraHudson Kamoga ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa Clouds Media. 

 

UONGOZI NA WAFANYAKAZI WA GLOBAL GROUP, unaungana na Wanatasnia wengine na Watanzania kwa ujumla katika kuifariji familia ya Mutahaba katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema – Ameen!

Maneno Mazito ya WAZIRI MKUU Msibani kwa RUGE, Yatakutoa Machozi!