
Hit Maker wa ‘One Ticket’ toka Nigeria amefunguka swala kubwa kuhusiana na ndoa kwasababu amekuwa akiona wenzake kila siku wanachukua maamuzi ya kuoa huku yeye yupo katika hali ya tofauti na wao.
Kupitia account yake ya Twitter amewaahidi mashabiki kwamba ni lazima mwaka 2019 na yeye ajiunge katika familia ya watu waliouaga ubachela,akimaanisha maisha ya ndoa.

Kizz Daniel anategemea kudondosha Album yake ya ‘No Bad Songz’ kabla ya mwaka huu kuisha na ‘One Ticket’ ni moja kati ya ngoma itakayopatikana kwenye Album hiyo.