
Rapa wa kike Cardi B ametimiza ndoto yake ya muda mrefu baada ya kutumia kipato chake kumnunulia mama yake zawadi ya nyumba yenye thamani ya Dola 600,000 (Sh bil. 1.5) ambayo ipo jijini New York.
Jumatatu Novemba 19, 2018, Cardi aliweka video mbili katika akaunti yake ya Instagram ambazo zilikuwa na maelezo yanayosomeka, “Imekuwa ndoto yangu ya kila siku kuja kumnunulia mama yangu nyumba, lakini kila nilipokuwa nahitaji sikupata yenye kuendana na pesa yangu,nimefanya kazi, nimefanya sana kazi na wakati huu nipo hapa. Nashukuru kwa kila mtu ambaye amenisapoti kwenye ndoto yangu ya utotoni kuja kuwa kweli, ‘kumnunulia mama yangu nyumba’!!…Usiniulize upuuzi, mimi ni mwanamke wa gharama”.
VIDEO ZA JUMBA HILO