×

Ben Pol: Skendo ya Kuachana Imekoleza Penzi Letu!

 

 

BENARD Paul ‘Ben Pol’ amefanya balaa kwenye wimbo wake mpya wa Sikukuu.

Ni wimbo mzuri ambao ameutoa katika muda muafaka kwani sikukuu ndio leo na mwaka mpya huo unakaribia!

Kabla ya kuachia wimbo huo, maneno mengi yalipita hapo katikati kumhusu Ben Pol. Kuna ambao walisema yupo bize na mpenzi wake Anerlisa Muigai kiasi cha kuupa kisogo muziki.

 

Juzikati, zikapita stori kuwa wameachana na mpenzi wake huyo na kusababisha gumzo mitandaoni.

Baada ya stori hizo, Risasi Vibes imezungumza na Ben Pol. Amezungumza mengi yahusuyo muziki pamoja na maisha yake na mpenzi wake huyo raiya wa Kenya:

Risasi Vibes: Nini kimekusukuma kutoa wimbo wakati huu wa sikukuu ya Krismasi?

 

Ben Pol: Nimefanya hivyo kwa ajili ya zawadi kwa mashabiki zangu na kuwatakia heri na ndipo niliona ni zawadi pekee kwao lakini pia ninazo mbili ambazo nitazitoa mwanzoni wa mwaka mpya.

Risasi Vibes: Vipi kuhusu sikukuu, japokuwa utatoa nyimbo lakini utakuwa hapa nchini au utaenda kusherehekea kwa mchumba wako Kenya?

 

Ben Paul: Nitakuwa hapa nchini na familia yangu, nikimaanisha mama yangu, ndugu zangu na mchumba wangu na mtoto wangu Mali. Kwa pamoja tutakuwepo hapa nyumbani.

Risasi Vibes: Vipi mchumba wako anamchukuliaje mtoto wako, maana wengine wanakuwa hawapendi watoto.

Ben Paul: Kwa kweli Anerlisa anampenda mtoto wangu sana kwa hilo siwezi kusema vibaya, yaani anamfanya kama mtoto wake.

 

Risasi Vibes: Vipi kuhusu mzazi mwenzio anachukuliaje mtoto anavyokuja kukaa na mchumba wako?

Ben Paul: Kwanza kabisa mimi sipendi kuwachanganya Ratifa ambaye ni mama wa mtoto wangu na mchumba wangu, yaani hata kama nitamuomba mtoto, sipendi mtu yeyote wa upande wa mama mtoto wangu ajue niko na nani na hiyo inaepusha mambo mengi sana kwa sababu hata kama Anerlisa akiwa Tanzania, sio wote wanaojua kuwa yuko hapa.

 

Risasi Vibes: Vipi kuhusu ndoa yenu maana najua mahari tayari!

Ben Paul: Watu wetu wanaotupenda wazidi kutuombea heri siku zote, muda si mrefu tutafunga ndoa.

Risasi Vibes: Ungependa kuongeza watoto wangapi kwa mchumba wako huyo?

Ben Paul: Siku zote nilikuwa nikitamani watoto wanne, hivyo nitaongeza watatu kwa mchumba wangu.

Risasi Vibes: Anerlisa anajua kuimba? Au ana kipaji hicho?

 

Ben Paul: Anajua kuimba sana na ana sauti nzuri sana lakini hapendi kuwa msanii kabisa, yaani ile mikikimikiki ya kupanda jukwaani haiwezi. Ataimba tu kujifurahisha au kunifurahisha mimi.

Risasi Vibes: Ile habari ya kuachana wewe na mchumba wako iliathiri vipi mahusiano yenu?

 

Ben Paul: Kwa kweli ilifanya mahaba yaongezeke maradufu kwa maana tulikuwa tukishangaa kwenye mitandao ya kijamii wanavyoandika, tunatumiana tunacheka sana.

Risasi Vibes: Ulishampeleka Anerlisa nyumbani kwenu Dodoma?

Ben Paul: Anakujua vizuri na karanga analima vizuri sana.

Risasi Vibes: Asante sana.

 

Stori: MEMORISE RICHARD

Leave a Comment