
Hit Maker wa ‘Science Student’ toka Nigeria, ‘Olamide’, ameahidi kuwapa mashabiki wake zawadi ya albam mpya kabla ya mwaka kuisha — Desemba.
Albam hiyo inajulikana kwa jina la YBNL Mafia na inategemewa kuingia sokoni tarehe 7 December mwaka huu.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo ameweka post ya cover la albam pamoja na maelezo yaliyoambatana na sehemu ya albam hiyo itakapopatikana na muda maalumu wa kuiachia , “YBNL MAFIA FAMILY !!!! Out next week.Dec the 7th only on iTunes,tidal,Spotify and alaba market for the street for obvious reasons init. “
