×

RIHANNA KWENYE MOVIE NA GAMBINO, TRAILER IPO HAPA – VIDEO

MUIGIZAJI Donald McKinley Glover Jr. ‘Chaldish Gambino’ na mwanamuziki maarufu duniani Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ wameachia trailer ya project ya filamu yao mpya ambayo wameicheza huko nchini Cuba mwezi Agosti, mwaka huu.

 

Filamu hiyo imepewa jina la Guava Island ambayo kipande chake kidogo cha video kimeshewa ambacho hakina ubora kutokana kilichukuliwa kwa camera kwenye screen kutoka kwenye show ya Pharos ya Donald  Gloves huko New Zealand.

 

Baadhi ya picha zilianza kusambaa mtandaoni Agosti 16, mwaka huu ndyo ikajulikana wawili hao wanatengeneza movie.

 

Filamu hiyo ya Chaldish Gambino pamoja na Rihanna, ‘Guava Island’ haijatangazwa tarehe kamili ya kuingia sokoni mpaka wakati huu.