×

CHRIS BROWN KUJA NA HII KALI NOVEMBA HII

Msanii wa R&B Chris Brown ametoa taarifa za kuwafurahisha mashabiki zake katika akaunti yake ya Instagram jana (Alhamisi November 29).

 

Taarifa hiyo ilikuwa inaongelea project mpya anayotaka kuja nayo itakayokwenda kwa jina la ‘Indingo’ lakini kilichowashangaza mashabiki ni kwamba post hiyo iliwekwa kwa muda mfupi halafu akaifuta mwenyewe.

 

 

Chris Brown amekuwa bize sana mwaka huu kwa sababu ameshafanya kolabo na wasanii wenzake akiwemo,Tory Lanez, Agnez Mo, Ella Mai na Trey Songz.

 

Albam ya mwisho ya Brown ilikuwa  Heart Break On Full Moon ambayo ilikuwa Double Album iliyokuwa na nyimbo 48 na mauzo yake ya wiki ya kwanza yaliiwezesha kukamata nafasi ya tatu katika albam bora 200 za Billboard.