×

CARDI B KAFUNGA MWAKA NA HII, AONGEA MAMBO 7 USIYOYAJUA

Rapa wa kike, Cardi B, pamoja na kutokea katika ‘kava ya jarida la Entertainment Weekly amefanikiwa kuwa Mtumbuizaji Bora wa Mwaka.

 

Katika jarida hilo amezungumza mengi kuhusu matamasha, muziki wake, ushirikiano na wasanii wenzake,  kumbukumbu  muhimu na mengine.

 

Mambo saba muhimu aliyoyafunguka kwenye jarida hilo ni:

1. Kuhusu  Tarifa ya Mashabiki  kumtaka Mariah Carey Kufanya kazi na Cardi B.

 

Alifunguka: “Nataka kufanya kazi na yeyote ambaye sijafanya kazi naye, nilisikia Mariah Carey anataka kufanya kazi na mimi nikashangaa.

 

2. Kumbukumbu muhimu na kubwa kwa mwaka 2018

 

Siku ambayo nimejifungua nilikuwa na hisia sana na sikuacha kulia kila wakati huku nawaza hivi hiki kitu ni cha kweli?”.

 

3. Albam yake kufikia Namba 1 kwenye Chart za Billboard 200

 

Ni kitu ambacho kilinipa furaha, nimejivunia, najiskia kwamba hakuna mtu ataniweka mbali na muziki wala kutofanya album bora”.

 

5: Tamasha kubwa alilofanya na akaridhika.

 

Nilipofanya tamasha Mtv EMAS lilikuwa tamasha langu kubwa la televishen la kwanza baada ya kujifungua na nikajisikia nataka kuona watu wata-react vipi kwa sababu baada ya albam yangu sikufanya matamasha ya muziki, nilikuwa na wasiwasi lakini mwisho lilimalizika vizuri ambavyo sikutegemea.”

 

6: Kufanya kazi na wasanii wenzake

 

Huwa napigiwa  simu na nashangaa mtu fulani anataka kufanya kazi na mimi, kama Bruno Mars anataka kufanya kazi na mimi, ‘naota au’?”.

 

7: Kitu anachokitarajia kufanya kwa mwaka 2019

 

Naangalia kufanya vyovyote  na chochote ambacho kitanisaidia, kuhusiana na  adui zangu ndiyo muda wao, nina ndoto zangu nadhani ndiyo muda muafaka wa kuyafanya hayo“.