
Rapa Meek Mill amefunguka kupitia CNN kuhusiana na nyimbo ya ‘What’s Free’ aliomshirikisha Jay-Z inayopatikana kwenye albam yake ya Championships iliyotoka Ijumaa, kwamba alifurahia suala la Jay kuingiza sauti yake kwenye albam japo aliwadis Kanye West na Trump.
Kwenye ngoma hiyo mstari huo aliowadis ulikaririwa kwamba Jay-z hakuwa anakubaliana na muunganiko wa Kanye West na Donald Trump kwenye kuijenga America kuwa kubwa tena.
Meek Mill alipoulizwa kuhisiana na kama alijua Jay-z amemdis Kanye kwenye nyimbo inayopatikana kwenye album yake alisema, “sidhani kama Jay-z alifanya vile kumdiss Kanye West, nadhani alikuwa anasema, ‘usiwape nafasi wakatutenga kama Michael Jackson na Prince.’”
Alipoulizwa kuhusiana na kumuuliza Jay-z kuhusiana na mistari yake kwenye hiyo nyimbo alisema, “Sijaongea naye lolote kuhusiana na hilo.Nilikuwa na ndoto za kufanya kazi na Jay kwenye maisha yangu, kupata nafasi ya kufanya kazi na mtu mkubwa wakati wote chochote alichofanya na kunipa mimi nimepaswa nipokee na nikikubali. Hicho ndicho alichokiwakilisha kwangu na nimekifurahia”.
Hata hivyo Jay-z alishafunguka kuhusiana na mstari huo kupitia akaunti yake ya tweeter kwa kukanusha kuwa hajamdis Kanye West.