
Baada ya rapa Drake kumaliza ziara yake ya muziki ya Three Migos ndani ya Atlanta Nov 18,boss wa Young Money ‘Lil Wayne’ amemtumia message iliyowashangaza mashabiki wengi na kumpongeza pia.
Kwenye kipande cha video Lil Wayne anaonekana akisema, “vipi Champaigne, hongera kwa ziara yako,we ni mtu mbaya sana, mafanikio mengi, upendo mwingi, pesa nyingi, yote mazuri unastahili kaka.”
Kwenye kipande cha video pia aliweza kutoa baadhi ya maneno ambayoo yaliwashangaza mashabiki weni lakini pia ilikuwa furaha kwa mashabiki wa pende zote mbili, “sipati picha tutakavyorudi kwenye stage pamoja, kufanya ziara yetu ya pamoja Drake vs. Tune au Lil Wayne vyovyote mtakavyoiita.Hongera sana”.Alimaliza Lil Wayne
Kumekuwa pia na tetesi ambazo zinasema kuna project ambayo itakuja January 2019 inayoitwa, ‘Wolf SZN’ ya Lil Wayne pamoja na Drake.
