×

Maamuzi ya Diamond na Tanasha Kwenye Mitandao ya Kijamii

 

SIYO siri kwa walio wengi kwamba Diamond Platnumz na mwanadada Tanasha kutoka Kenya ni wapenzi kwa sababu wawili hao wameshaweka wazi kuhusiana na hilo.

 

Desemba 17 mwaka huu, mwanadada Tanasha alifunguka kwamba endapo hawataonekana katika mitandao ya kijamii wakiwa pamoja ni kwamba wameamua kuweka mahusiano yao faragha.

 

Tanasha ameweka post inayosomeka, “D na mimi tumeamua kuweka mahusiano yetu binafsi nje ya mitandao ya kijamii, tunatazama mambo yajayo na furaha yetu, muda ukifika tutaweka mahusiano yetu hadharani tena”.

 

Lakini post hiyo ilikuwa imeandamana na maelezo yanayosomeka, “Acha niweke mambo sawa, mimi na D tumefikia maamuzi baada ya kuona kwamba ni mapema sana kuweka mahusiano yetu hadharani kwenye mitandao ya kijamii kwa wakati huu. Kwa hiyo tumeamua kuweka mahusiano yetu faragha kwa muda mpaka tuhisi kwamba tunaweza kwenda hadharani kwa mara nyingine.Mungu awabariki nyote” aliandika Tanasha kwenye post yake ya Instagram