×

Video: Maono Ya Marehemu Bilago Mbunge Juu Ya Kikokotoo

Aliyekuwa  Mbunge wa Jimbo la Buyungu, wilayani Kakonko mkoani Kigoma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Marehemu Kasuku Samson Bilago aliwahi kuchangia bungeni akiomba kikokotoo kiingie kwenye mswada wa kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na siyo kwenye kanuni.

Aliomba kikokotoo kianze na wanachana wapya baada ya mifuko hiyo ya jamii kuunganishwa na siyo kwa wanachama wa zamani.