×

Mtanzania Amtwanga Mchina Kwa ‘Knockout’

Mwanafunzi Mtanzania, Isaack Ibrahim Emmanuel (kushoto) akitangazwa mshindi baada ya kumpiga kwa ‘KO’ Mchina Zi xiǎo yún yǔ.

Mwanafunzi wa Tanzania anayesoma nchini China, Isaack Ibrahim Emmanuel,  juzi ameibuka kidedea katika mchezo wa kick boxing baada ya kumpiga kwa ‘knockout’ (KO) Mchina Zi xiǎo yún yǔ mjini Jillin.

 

Isaack ambaye anasomea uhandisi wa Madawa au ‘Pharmaceuticals Engineering’ katika Chuo Kikuu cha Liaoning jijini Shenyang, ameushangaza umati wa Wachina kwa kumgaragaza Zi ambaye hajawahi kupigwa hata siku moja.

Isaack akimrushia makonde mazito Mchina.

 

Mpambano huo wa kilo 60 umempa umaarufu mkubwa Isaack kiasi hata waandaaji wa mapambano wameanza kupigana vikumbo kumtaka acheze mapambano zaidi.

 

Akiwa na uwezo wa kutumia kwa kasi ya ajabu miguu na mikono yote, wataalamu wa mchezo huo wamemtabiria makubwa kijana huyu wa kutoka mkoani Mwanza.