×

Ukitaka Kufanikiwa 2019, Fanya Hivi!

Mtumishi wa Mungu, Bishop Paul Chaba wa Kanisa la PWCT lililopo Nata wilayani Nyamagana Mwanza amesema ili mtu yeyote aweze kufanikiwa katika mwaka 2019 anatakiwa kumuomba na kumtegemea Mungu pamoja na kufanya kazi kwa bidii hii itasaidia kutimiza malengo yake.

Chaba amesema watu wengi wanashindwa kufikia malengo yao kutokana na kumuacha Mungu na kumfuata shetani jambo ambalo linamchukiza Mungu.

Aidha amewataka waumini wa kanisa hilo na wakristo wote kufanya kazi kwa bidii pamoja na kumtegemea Mungu katika kazi zao ili waweze kufanikiwa na kutimiza malengo yao ya mwaka 2019.