Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, amejikita kusapoti ujenzi wa ofisi za CCM kata katika jimbo hilo ili kurahisisha huduma kwa wanachama wa chama hicho.
Mabula amesema anatambua kuwa umuhimu wa chama cha Mapinduzi (CCM) kujenga ofisi zake kila kata jambo ambalo litasaidia wanachama kupata huduma karibu na maeneo yao.
Mbunge Mabula ametoa mabati bando nne zenye mabati 72 katika kata ya Butimba na Pamba ili kukamilisha ujenzi wa Ofisi hizo.