×

MTOTO WA KALAJA BAADA YA KUFELI ATIWE MOYO

Kajala, Paula

Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka hivi karibuni, mtoto wa msanii maarufu Kajala, Paula imefahamika kuwa amefeli na baadhi ya watu kumsakama. Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo amelazimika kumtetea mtoto huyo na kusema yafuatayo:

Nimelazimika kama mzazi kuliongelea suala hili; Mashambulizi yaliyoelekezwa kwa mtoto wa Kajala, Paula, sababu tu hakufaulu mtihani wa Taifa kidato nne ni ukatili unaoweza kuleta madhara makubwa kisaikolojia kwa mtoto.

 

Napenda tu kuwakumbusha kuwa mwanamuziki Jeniffer Hudson mara ya kwanza aliposhiriki Mashindano ya American Idol, alishindwa na jaji akamwambia; “Safari yako imeishia hapa!”

 

Jambo ambalo jaji hakufahamu ni kwamba huyu Jeniffer ndiye baadaye kupitia milango mingine alikuja kuwa mwanamuziki maarufu ulimwenguni akishinda tuzo nyingi sana.

 

Mimi ingawa nilikuwa na ndoto ya kuingia chuo kikuu, nilifeli Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, sikusoma sekondari, wenzangu wakandelea.

 

Sababu hiyo niliitwa mjinga na hata kutukanwa, lakini leo hii ni Shigongo mnayemfahamu, anasoma chuo Kkkuu kilekile alichoshindwa kujiunga nacho wakati ule sababu alionekana mjinga na zaidi sana amewaajiri waliofaulu mtihani wa Darasa la Saba na kwenda Sekondari wakimwacha yeye kijijjni.

 

Ndugu zangu, Mungu yupo na ndiye anayejua hatima za kila mmoja wetu, si vizuri kumhukumu mtoto huyu sababu eti kafeli, wangapi tulifeli?

Badala ya kumshambulia tumtieni moyo, kwani hakuna ajuaye, miaka michache ijayo mtoto wa Monaliza anyesifiwa leo anaweza kuwa mfanyakazi wa Paula, tukaona aibu.

Kwa Paula na mama yake nasema; sikiliza, achana na maneno ya watu, kazi yako ni moja tu sasa; kuuthibitishia ulimwengu kuwa wewe si mjinga kama wanavyochukuliwa, jipange upya na uendelee kufukuzia ndoto zako na MUNGU ATAKUWA NA WEWE HADI MWISHO.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club