×

Waziri Jerry Silaa Atangaza kuvunja bodi TTCL, TPC na UCSAF

Siku kadhaa tangu Rais Samia Suluhu Hassan atengue uteuzi wa wenyeviti wa bodi katika baadhi ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Waziri Jerry Silaa ametangaza kuvunja bodi za taasisi hizo.

Bodi za taasisi zilizovunjwa ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, hatua hiyo imekuja kutokana na utenguzi uliyofanywa na Rais Samia wa kuwaondoa wenyeviti wa bodi wa taasisi hizo.

TANZANIA YAMALIZA NGWE ya KWANZA ya MICHEZO ya OLIMPIKI ya KUOGELEWA – SOPHIA APEPERUSHA BENDERA….

Leave a Comment