×

Video: Dkt Abbas Afunguka A-Z Mipango ya Serikali 2019

 

MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassani Abbas, mapema jana amepata fursa ya kutembelea ofisi za Global Group na kuzungumzia mipango ya serikali kwa mwaka 2019 ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya 69 nchini na ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia treni ya umeme.

 

Kuhusu Watu wanaokosoa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa ndege, Dk Abbas amesema hao ni wa kupuuzwa na kinachofanyika sasa ni kutekeleza ahadi ya serikali ya awamu ya Tano.

 

Katika hatua nyingine Dk Abbas amesema ataendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali nchini lengo ni kuwaeleza wananchi yanayofanywa na serikali pamoja na kupokea kero na kuziwasilisha kwenye taasisi husika.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club