
Mwili wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa umefika nyumbani kwake jioni ya leo Julai 28, 2020 katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara.
Mwili wa Rais Mstaafu, Mzee Benjamin Mkapa uliwasili leo katika Uwanja wa Ndege wa masasi Mkoani Mtwara kwa Helkopta ya Jeshi ukitokea Dar es Salaam na kupelekwa nyumbani kwao, Lupaso kwa ajili ya ibada ya mazishi ambayo yatafanyika kesho.