×

JPM Aeleza Kwa Nini Hakumteua DPP Kuwa Jaji – Video

RAIS  John Magufuli amesema miongoni mwa majina aliyopelekewa yakiwa yamependekezwa kuteuliwa kuwa majaji ni Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP)  Biswalo Mganga ambaye hakumteua.

 

Hayo aliyasema leo (Jumanne) Januari 29, 2019  wakati akihutubia baada ya kuwaapisha majaji, wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambao aliwateua juzi (Jumapili)  ambapo amesema licha ya kupelekewa jina hilo hakuliteua huku akitaja sababu za kutomteua kuwa jaji.

 

“Ujaji ni cheo kikubwa, unampa mtu madaraka ya kwenda kuamua, na ukishamteua umemaliza, yeye kazi yake inabaki ni kuamua tu. Ndiyo maana unatakiwa kuwa makini sana.  – Magufuli.

 

Kazi ya kuteua ni ngumu, pengine unatakiwa kumtanguliza Mungu, nilikuwa na majina 58 ya mwaka jana na mengine 65 ya mwaka huu na mengine kutoka sehemu nyingine, kazi ya ujaji ni kubwa kwa hiyo uteuzi wake unatakiwa kuwa na uangalifu. – Magufuli.

 

Uwe mahakama ya chini au ya juu haijalishi, ukifanya kazi kwa weledi utateuliwa tu kuwa jaji, nyinyi majaji mnapaswa kuwa vioo kwa kuwa manatazamwa na wengi, na wengi watatoa hukumu zao, kazi zenu za kutoa haki zina changamoto na ugumu sana. – Magufuli.

 

DPP alikuwa ni moja ya watu waliopendekezwa kuwa majaji, ila sijamchagua maana yeye ndiyo anapeleka mafisadi mahakamani, acha kwanza awasimamie mafisadi. Jinsi muda unavyokwenda na kazi zinavyoendelea nitaendelea kuwateua majaji haswa ukizingatia kwa sasa kuna Mahakama ya Mafisadi, hivyo ipo haja ya kuwaongezea majaji. – Magufuli.

 

Ninayazungumza haya ndugu zangu Waheshimiwa Majaji ili muelewe mna nafasi kubwa ninyi kuwa vioo. Jamii inawatazama.Unapotazamwa na wengi, ‘assessment’ pia inakuwa ni ya watu wengi. Na unapopewa nafasi ya kusimamia haki ni nafasi ngumu sana yenye ‘challenge’ nyingi.  – Magufuli.

 

Inahitaji kweli… kwa dhati kabisa kumtanguliza Mungu. Kazi zenu zina vishawishi vingi, zina lawama nyingi. Lakini ukisimama katika haki, mtafanikiwa sana. Na ndiyo maana nasema Mheshimiwa Jaji Mkuu, Majaji wengi wanafanya kazi nzuri sana. Na mimi nawapongeza sana.  – Magufuli.

 

Kamishna wa kazi, Ndugu Malata, kule kulikuwa na mambo ya hovyo sana, ameyashughulikia, siku hizi watu wanapiga kelele sana ‘vibali vya kazi’, lakini ninaambiwa anafanya kazi, zamani walikuwa wanaomba vibali wanakuja kujenga barabara kumbe hawajui hata ‘engineering’ (uhandisi). – Magufuli.

VIDEO: MSIKIE MAGUFULI AHAPA AKIFUNGUKA