Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo, amemkabidhi Mkuu wa wilaya ya Meru Jerry Muro Vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga vya awamu ya pili.
Vitambulisho hivyo zaidi ya elfu 20 vilitolewa na mkuu wa mkoa mbele ya wakurugenzi wote wa halimashauri za Meru na Arusha na kushuhudiwa na makatibu kata na wenyeviti wa vijiji walio kuwepo katika ukumbi wa mikutano wa halimashauri ya Arusha.
Katika makabidhiano hayo Gambo amewahimiza watendaji kata kuongeza spidi ya utoaji wa vitambulisho hivyo na kuhimiza uaminifu wa upelekaji wa fedha za vitambulisho hivyo benki.