Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwauwa majambazi watatu waliokuwa na silaha ya moto katika maeneo ya Nyakabungo kata ya Isamilo wilayani Nyamagana Mwanza.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokeoa leo Feb.6.2019 majira ya saa 8 usiku baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema kutokana na kuwepo kwa majambazi katika eneo hilo.
jambo lilofanya askari waliokuwa doria kuwahi eneo la tukio ambapo majambazi hao walianza kurusha risasi kuelekea walipo askari jambo lililofanya kuibuka kwa mpambano mkali na mwisho Askari kufanikiwa kuwaua Majambazi watatu hapo papo.