×

WASANII GLOBAL TV KUIPEPERUSHA BENDERA FAINALI SZIFF

LEO ndiyo leo! Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, ya utoaji wa tuzo za Sinema Zetu Fil festival (SZIF) imewadia ambapo wasanii kibao wa tasnia ya filamu za Kibongo pamoja na wadau wengine, watajumuika katika Ukumbi wa Mlimani City kujua mbivu na mbichi.

Kwa taarifa yako, wasanii wawili, Sango Johanes na Rhoida Richard ambao filamu zao huonekana kupitia chaneli ya Global TV Online kila Jumamosi, ni miongoni mwa waliopenya na kuingia hatua ya fainali ambapo leo watakuwa wakichuana na wakali wengine kibao kwenye Bongo Movies.

Sango anawania tuzo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume na Rhoida anawania tuzo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike wote wawili wakiwa wameingia kupitia filamu ya Ardhi ya Damu, ambayo pia ilioneshwa Global TV Online.

 

Macho na masikio yote kwa sasa ni Mlimani City ambapo mashabiki wa filamu watashuhudia Sango na Rhoida, wakiipeperusha bendera ya Global TV Online.

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART TWO)