
Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival, (SZIFF 2019), zimefanyika jana Februari 23 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Tuzo hizo zimeacha historia baada ya Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike kwenda kwa mtoto Flora Patience Kihombo kupitia muvi ya ‘Kesho’ na kuwamwaga waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania, Yvone Cherry ‘Mwanalisa’ na Wema Sepetu.

Pia Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume imekwenda kwa mtoto, Rashid Msigala kupitia muvi ya ‘Kesho’ akiwamwaga Maulid Ally, Madebe Lidai, Hemed Suleiman, Peter Paul, Hasan Kazoa, Mack Adam, Salim Ahmed na wengine.

Hapa Chini ni washindi wa Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival, (SZIFF 2019)
1. MUIGIZAJI BORA WA KIUME: Tuzo imekwenda kwa Rashid Msigala kupitia filamu ya ‘Kesho’.
2. FILAMU BORA YA MWAKA WORLD CINEMA: Tuzo imekwenda kwa filamu ya Pihu kutoka India.
3. MUIGIZAJI BORA WA KIKE: Tuzo imekwenda kwa Flora Patience Kihombo kupitia movie ya ‘Kesho’.

4. Filamu Bora yenye Maudhui ya Kitaifa – Filamu iliyoshinda ni SIYABONGA kutoka kwa Salim Ahmed a.k.a Gabo Zigamba
6. Sinema Zetu imetoa tuzo kwa filamu ambazo hazijapata tuzo katika vipengele vingine lakini zimefanya vizuri katika mikoa mbalimbali.

7. MSHINDI – Tuzo ya Mtu Aliyetukuka katika tasnia ya Filamu Tanzania inakwenda kwa Mzee Majuto (ambaye kwa sasa ni marehemu). Tuzo hii imetolewa na majaji.
8. Filamu Bora upande wa Filamu Fupi – Filamu iliyoshinda ni SUPA MAMA

9. Muigizaji Bora wa Kike katika World Cinema – Washindi ni wawili, Leena Alam kutoka Afghanstan na Myra Vishwakarma kutoka India.
10. Makala Bora – Mshindi ni Adam Juma kupitia makala ya AMKA – Muigizaji Bora wa Kike katika World Cinema – Washindi ni wawili, Leena Alam kutoka Afghanstan na Myra Vishwakarma kutoka India

11. Mchekeshaji Bora katika Filamu Ndefu – Mshindi ni Madebe Lidai kupitia filamu ya ‘MAMA MWALI’
12. Mwandishi Bora wa Muswada – Filamu iliyoshinda ni ‘SUPA MAMA’, mshindi akiwa ni Christina Pande

13. Mhariri Bora wa Filamu Fupi – Mshindi ni Ibrahim Jabir kupitia filamu ya ‘TAMAA’.
14. Mpiga Picha Bora Filamu Ndefu – Filamu iliyoshinda ni T-JUNCTION mshindi akiwa ni Lister Millado.

15. Mpiga Picha Bora katika Filamu Fupi – Mshindi ni Adam Juma katika filamu ya ‘TAMAA’.
16. Muziki Bora wa Filamu Ndefu – Filamu iliyoshinda ni ‘DEMA’ mshindi akiwa ni Khatwab Khamis.
17. Muziki Bora World Cinema – Filamu iliyoshinda ni ‘THE SILENT REVOLUTION’
18. Muziki Bora wa Filamu Fupi – Filamu iliyoshinda ni SISI NA WAO.
PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL