Rais MAGUFULI Amuaga RUGE kwa Mara ya Mwisho (Picha +Video)
Global Publishers March 2, 2019
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali na maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mwasisi na Mkurugezi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, aliyefariki dunia Februari 26, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Magufuli leo Machi 2, 2019 aalifanya hivyo katika viwanja vya Karimjee, akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete; mawaziri, wabunge na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa ndugu na familia ya Marehemu Ruge Mutahaba alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa baadhi wananchi waliofikika kutoa heshima zao kwa Marehemu Ruge Mutahaba.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine alipoongoza maelfu ya waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019 Sehemu ya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa marehemu ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019