
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media Group, Ephraim Kibonde utawasili leo usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (JKNIA) na utapelekwa Hospitali ya Jeshi, Lugalo kuhifadhiwa. Taratibu za mazishi zitafanyika nyumbani kwake Mbezi na Jumamosi, Machi 9, 2019 ambapo ataagwa na kuzikwa.

Ndugu, jamaa na marafiki wa Kibonde, wameungana na waombolezaji nyumbani kwa wazazi wa marehemu huyo Mbezi-Africana jijini Dar es Salaam.

Hiyo inafuatia msiba huo uliomkuta mtangazaji huyo aliyepatwa na umauti leo asubuhi alipokuwa jijini Mwanza alipokuwa njiani kutoka mkoani Kagera kumzika bosi wake, Ruge Mutahaba.


Tayari watu wa Mwanza wameshatoa heshima za mwisho kwa marehemu Ephrahim Kibonde na tayari mwili unaelekea Airport kuanza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam kwaajili ya maziko.




