KIBONDE AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI LEO (PICHA +VIDEO)
Global Publishers March 9, 2019
SHARE THIS:
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media, Ephraim Kibonde ukishushwa kwenye makaburi ya Kinondoni leo.Waziri wa habari, utamaduni na michezo, Harrison Mwakyembe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kibonde.Wabunge akiwemo Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Zitto Zuber Kabwe na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haul ‘Prof. Jay’ wakiwa wakiweka shada la maua kama ishara ya kumuaga mpendwa wao.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka shada la maua.
Mwili wa Mtangazaji wa Clouds Media, Ephraim Kibonde umezikwa katika makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam huku mamia ya waomboleaji wakijitokeza kumzika.
Mwili wa mtangazaji wa Clouds, Ephraim Kibonde ukiwa juu ya kaburi kabla ya kuzikwa.
Waziri wa habari, utamaduni na michezo, Harrison Mwakyembe amewaongoza mimia ya waomboleaji kuuzika mwili wa Kibonde huku pia wabunge akiwemo Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Zitto Zuber Kabwe na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haul ‘Prof. Jay’ wakiwa miongoni mwa waombolezaji waliopata fursa ya kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu Ephraim Kibonde.
Mama wa Marehemu Kibonde na mumewe mzee Kibonde wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao Kibonde.Watoto wa Kibonde wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao.Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi, Gardner G Habash, kushoto akiwa na mtoto wa Ephraim Kibonde.Watoto wa marehemu wakijiandaa kuweka shada kwenye kaburi la baba yao.