×

LOWASSA ATUA MONDULI, APOKELEWA NA WANA-CCM (PICHA+VIDEO)

Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akipokelewa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Monduli.

WAZIRI mkuu mstaafu, Edward Lowassa,  ametua wilayani Monduli na kupokewa kwa shangwe na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) ambao wamekusanyika viwanja vya chama hicho.

…Akiwasalimia wananchi wa Monduli.

Lowassa alifika Monduli majira ya saa 7:34 na kushuka kwenye gari na kupokewa na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga.


Baada ya kushuka kwenye gari, Lowassa aliwapungia mkono wafuasi wa CCM ambao walilipuka kwa shangwe na vigelegele.


Baadaye alikwenda moja kwa moja ofisi za CCM wilayani Monduli kwenye kikao maalum ambacho alishiriki pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole.
Baada ya kikao hicho ambacho kilijumuisha wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Monduli, Lowassa alikabidhiwa kadi ya CCM.