×

EXCLUSIVE: Baada ya Kifo cha Kapteni Komba, Shuhudia Hiki! – Video

Ikiwa ni miaka minne imepita tangu kufariki kwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kepteni John Komba, Global TV imeitembelea familia yake nyumbani wanapoishi na kuzungumza na mkewe.

 

Global TV imejionea ujenzi wa kisasa unaoendelea nyumbani hapo ambapo ndani yake kutakuwa na Makumbusho ya kumuenzi mwanasiasa huyo mwanamuziki aliyekuwa akitunga na kuimba nyimbo za CCM.

 

Kapteni John Komba alifariki dunia, Februari 28, 2015 na kuacha pigo kubwa kwa familia yake, CCM, Jimboni kwake (Mbinga Magharibi) na Bendi aliokuwa akiitumikia ya T.O.T chini na Taifa zima kwa ujumla.

 

Kupitia Kipindi hiki Maalumu, Global TV imekuanikia mengi usiyoyajua kuhusu Kapteni Komba enzi za uhai wake ambapo mjane wa nguli huyo anafunguka.

TAZAMA VIDEO HII