×

MAMA AMLILIA MUNGU, “NIMEVIMBA TUMBO, SIONI, MOYO UNANITESA” – VIDEO

Bi. Selina Izack, mkazi wa Bunju A, Mtaa wa Baharia, mama anaesumbuliwa na tatizo la moyo, kisukari na vidonda vya tumbo, yupo kitandani kwa mwaka wa 18 sasa, hali iliyosababisha kuwa na ulemavu wa macho.

 

Kutokana na hali hiyo, mumewe amemkimbia, hivyo anahangaika kitandani peke yake. Madakatari wamemwambia anatakiwa awe na kiasi cha Tsh milioni moja ili atibiwe. Selina, kupitia Global TV, amemuomba RC Paul Makonda, amsaidie ilinaweze kupatiwa matibabu.

 

Kwa msaada na mchango wako ili aweze kupata matibabu unaweza kutumia namba
0713044060.