×

Pierre Liquid Apewa Tiketi ya Ndege Kwenda AFCON Misri – VIDEO

Mchekeshaji Peter Mollel ‘Liquid Master’ au ‘Pierre’ akisalimia wabunge leo baada ya kutambulishwa.

MCHEKESHAJI Peter Mollel ‘Liquid Master’ au ‘Pierre’, anayetikisa mitandaoni ameahidiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kupewa tiketi ya ndege kwenda kushangilia timu ya soka nchini Taifa Stars katika fainali zitakazofanyika nchini Misri mwezi juni mwaka huu.

Pierre akiwa na baadhi ya wabunge jijini Dodoma leo.

Kassim Majaliwa alisema hayo wakati msanii huyo alipotembelea Bungeni jijini Dodoma leo, Aprili 3, 2019.