×

Rais MAGUFULI Afungua Kituo cha Afya Mbonde, Mtwara – Video

Rais Dkt. John Magufuli amefungua Kituo cha Afya cha Mbonde Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara. Ni moja ya Vituo vya Afya 13 vilivyojengwa Mkoani Mtwara katika Awamu ya Tano na ni miongoni mwa Vituo vya Afya 352 vilivyojengwa nchi nzima katika Awamu hii ya Tano.

“Tumefanikiwa kujenga Vituo vya Kutolea Huduma za Afya 352 ambavyo vimejumuisha Hospitali za Halmashauri 9, Vituo vya Afya 304 na Zahanati 39 kwa gharama ya shilingi Bilioni 184.

“Nchi yetu tangu tumepata uhuru mwaka 61, tulikuwa na hospitali za Wilaya 77 tu, mbali na vituo hivi vinavyozinduliwa leo, vipo vituo vipya vinajengwa! Mfano kuna Hospitali mpya za Wilaya 67 zinajengwa. Mtwara mtapata Hospitali 3, huenda tukiendelea hivi itafikia kila Wilaya kuwa na Hospitali na nyingine mbili.

 

“Tukienda kwa mwendo huu, ninauhakika, kwa muda mfupi uliobaki, huenda kila Wilaya ikawa na hospitali mbilimbili,” amesema Magufuli.