×

Hakuna MIMBA za MAGEREZANI / Wafungwa Hawaruhusiwi Kuburudika! – Video

NI kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma ambapo leo ni kikao cha 12 katika mkutano wa 15 wa bunge la 11.

 

Leo wizara ya Katiba na Sheria itawasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020, na Wabunge wataendelea kuchangia ambapo tayari bajeti ya ofisi ya Rais TAMISEMI Pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, zimepitishwa bungeni kwa mwaka wa fedha 2019/2020, vikao hivi vya bunge vimeanza mapema April 2 mwaka huu.

Na kikao cha leo kimeongozwa na mwenyekiti wa Bunge Andrew John Chenge huku mbeba siwa akiwa Elia Mbise.