×

Arsenal, Chelsea lao moja, Kusaka tiketi ya nusu fainali Europa leo

ARSENAL na Chelsea leo zinasaka tiketi ya nusu fainali wakati zitakapotinga kibabe katika viwanja tofauti kwa mechi za marudiano za robo fainali ya Ligi ya Europa. Miamba hiyo miwili inayopewa nafasi kubwa kutwaa taji hilo msimu huu inaingia kwenye mechi za marudiano zikiwa na mtaji wa kushinda mechi za mwanzo.

 

Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Napoli wakati timu hizo mbili zilipokutana kwenye Uwanja wa Emirates, wiki iliyopita.

Wakati Chelsea kwa upande wao walipata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Slavia Prague ya Jamhuri ya Cech. Arsenal sasa inaifuata Napoli kwa mchezo wa marudiano ugenini kwenye Uwanja wa San Paulo mjini Naples.

 

Timu hiyo inahitaji sare, ushindi au ifungwe chini ya mabao mawili ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Kwa upande wa wapinzani wao, Napoli wanatakiwa kushinda zaidi ya mabao mawili kwa kutegemeana kama haitaruhusu bao ili kusonga mbele.